Sunday, May 8, 2011

OSAMA hakurudisha mipira iliyoingia kwenye uzio wa jumba lake...



Katika maisha ya kawaida mitaani tumeshuhudia viwanja vingi karibu na makazi ya watu(football,cricket n.k)nyakati nyingine wakati wa mchezo mipira imekua ikifika kwenye makazi hayo ya watu na wahusika kuirudisha kwenye uwanja(hapa kama utakutana na wahusika wapenda michezo)lakini hilo pia lilijiri kwenye makazi ya aliyekua kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha AL-QAEDA bwana OSAMA BIN LADEN kwani watoto waliokua wakicheza mpira wa CRICKET nje ya uzio wa jumba lake pindi mipira inapokua inaingia ndani ya jumba hilo basi hupewa fedha kwa ajili ya kununua mipira mingine na si kurudishiwa au kuingia kuchukua.kinara huyo wa AL-QAEDA hakutaka usumbufu katika maficho yake na ndo maana alitumia fedha kurudisha mipira hiyo.mipira hiyo inasemekana ilikua na thamani ya pauni 2.50 kwa mujibu wa maelezo ya mkazi mmoja wa eneo hilo.mtu mmoja alisema aliitupa karibu mara mbili mipira yake na kuvuka uzio huo wenye urefu wa futi 18,ambapo awali hakuwa akifahamu kwamba humo ndani anaishi OSAMA(54).

No comments:

Post a Comment

Popular Posts