
Studio ya CASH MONEY RECORD inaweza kuwa ndo nembo halisi katika historia ya muziki huko kwa OBAMA(marekani)kwa kuwa na wasanii wengi pengine kuliko zote zilizowahi kuwika na kufanya vizuri katika miondoko ya hip hop.Birdman amekizolea umaarufu na kujikuta akimiliki utajiri mkubwa anaofikia dola milioni 400(billioni 600 za madafu)kupitia lebo hiyo.BIRDMAN mzaliwa wa NEW ORLEANS,LOUISIANA,alianzisha CASH MONEY kwa kushirikiana na kaka yake RONALD'SLIM'WILLIAMS mnamo mwaka 1989,ambapo licha ya kuwa navipaji vingi aliendelea kuwa mwanamuziki na prodyuza huku akiwasaidia kuwatoa kimuziki wakali kama LIL' WAYNE'wizzle' na JUVENILLE kupitia lebo hiyo.akiwa kwenye kiwango cha juu mwaka 2000 alifanikiwa kuzoa dola million 25 baada ya kushinda tuzo ya wimbo bora wa hip hop kupitia ngoma yake ya NO 1 STUNNA na kuwafunika wakali wengine kibao wa miondoko hiyo hapo kama JIGGA'jay z' na ANKEL SNOOP DOGGY.jarida la forbes toleo la mwezi uliopita liliandika kuwa CASH MONEY na uhakika wa kuweka kibindoni zaidi ya dola 100 kwa mwaka kupitia kazi zinazofanyika mjengoni humo jambo ambalo lilipingwa viikali na mkali huyo kabla ya kuombwa radhi na chombo hicho cha habari.katika kuweka sawa mambo BIRDMAN alisisitiza kwamba akiwa na umri wa miaka 22 tayari alikua na mkwanja unaofikia dola millioni 40 na sasa ni mtu mzima anayetengeneza mpunga wa maana zaidi ya huo ulioanishwa na jarida la forbes.mkubwa anamiliki eneo lenye thamani ya dola millioni 30 huko MIAMI,huku mwenyewe akifafanua kuwa kila baada ya miezi 6 hununua magari mapya 100 na kuacha yote ya zamani.matumizi mengine ni pamoko na cheni za thamani mikanda,pete,heleni(puli)na meno ya bandia kama mapambo tu.mwaka wa kimbuka cha KATRINA mtu mzima alipoteza nyumba 20 na magari 50 zikiwemo MAYBACH 2 na FERRARI 4.kwa ufupi huyo ndo BIRDMAN,THE BOSS WA CASH MONEY.jina kamili ni BRYAN WILLIAMS kazaliwa FEBRUALY 15,1969 hadi sasa ana miaka 19 kwenye gemu.
No comments:
Post a Comment